KUYUMBA kwa uchumi ni miongoni mwa sababu ya migogoro kuanzia ngazi ya familia

Mtaalam wa masuala ya upangaji wa bajeti kuanzia ngazi ya familia kutoka katika Shirika lisilokuwa la Kiserikali la ELIMISHA Festo Sikagonamo, amesema ili kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye ngazi ya familia ni muhimu wanandoa wakapanga bajeti ya familia yao kwa pamoja yenye mlengo wa kijinsia. Amesema bajeti ya aina hiyo itasaidia familia kuwa yenye furaka kwa sababu mke na mume wakishirikiana kupanga bajeti watafanikiwa kutekeleza majukumu yao kwa pamoja na kuepukana na msongo wa mawazo. Aidha, amesema kufanya hivyo wanafamilia wataepuka baadhi ya matatizo kama vile ugomvi, kutoaminiana na vipigo ambavyo vimekuwa na madhara makubwa ikiwemo kusababisha vifo. Baadhi ya migogoro inayotokea kwa wanandoa chanzo kikubwa huwa kuyumba kiuchumi ukiyumba, wanafamilia huishi kwa kuviziana na huishia kwenye ukatili. Mwanaume hufikiri fedha za matumizi anazoziacha nyumbani huenda mke wake anatumia vibaya, wakati huo mwanamke naye hufikiri mume anapata kipato kikubwa, lakini hakifiki nyumbani kwa kuwa hawajatengeneza bajeti ya pamoja na hakuna utaratibu wa kupanga kwa siku, wiki na mwezi. Sikagonamo amefafanua kuwa bajeti inaweza kuwa msaada wa kukabiliana na ukatili wa kijinsia na kuokoa, maisha ya wanandoa kutokana na msongo wa mawazo, lakini pia kuleta furaha ya maisha. Kwa mujibu wa Sikagonamo, miongoni mwa faida ya upangaji bajeti yenye mlengo wa kijinsia ni kuepusha migogoro ya kugombania mali kwa madai kuwa mume au mke wanaingia kwenye ugomvi kwa sababu wanategemea mali hizo kuendesha maisha badala ya kufanya shughuli za uzalishaji mali. Amesema kwa udadisi waliofanya asilimia 75 ya makundi ya wanawake na vijana hawana elimu ya upangaji bajeti hali inawakwamisha jitihada za kutimiza malengo yao ya kujikwamua kiuchumi. Pamoja na hayo kuna tatizo jingine la wanawake kuwa na elimu ya kupanga bajeti, jambo linalosababisha fedha wanayopewa kama mtaji wa biashara kushindwa kuwasaidia na kurudi kuwa tegemezi na mtumwa kwakuwa haruhusiwi kuhoji kipato cha mumewe. “Uchumi ni miongoni mwa eneo linalochangia ukatili wa kijinsia kutokana na ukosefu wa elimu ya upangaji bajeti ndani ya familia kwa kiasi kikubwa wanaume ndio huwakatili wake zao hususani wasiokuwana vipato kwa maana ni mama wa nyumbani ili kukabiliana na vitendo hivyo elimu ya upangaji yenye mlengo wa kijinsia inahitajika,” amesema Sikagonamo.   Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, kati ya wanawake 10, saba wamefanyiwa vitendo vya ukatili wa uchumi na vipigo. Debora Mwanyanje Mtaalamu wa masuala ya jinsia kutoka Shirika la ELIMISHA, amesema ameshuhudia ndoa nyingi zikiharibika kutokana na ukatili wa kiuchumi, mume kushindwa kuhudumia familia na kumuachia jukumu mwanamke hali inayosababisha msongo wa mawazo na wakati mwingine mtu kulazimika kunywa sumu. Amesema kina mama wengi hulazimika kuingia kwenye madeni ili mradi akidhi mahitaji ya familia yake kutokana na waume zao kuwatekeleza wakikwepa majukumu kutokana hali hiyo huchangia msongo wa mawazo. Regina Sanga Mkazi wa Ilolo anayajishughulisha na kilimo cha mboga, amesema amekuwa msaada mkubwa kwa familia yake kwani licha ya mume wake kufariki dunia miaka kadhaa iliyopita amejitahidi kusomesha watoto na sasa wanajitegemea kwa vipato vyao. Amesema maisha yake huenda yangekuwa mazuri zaidi endapo angekuwa na elimu ya upangaji wa bajeti kuanzia ngazi ya familia angeweza kuzitumia vyema fedha anazozipata kwenye biashara yake ya kuuza mboga. Baadhi ya wanaume wamelalamikia wake zao kutokuwa na nidhamu ya fedha wanazoachiwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani wakidai hupeleka kwenye vikoba na upatu. Miongoni mwao amesema kila siku anamuachia Sh 5,000 kwa siku lakini haandai chakula kinachoendana na hela hiyo na kwamba amebaini mkewe ana matumizi mengine na fedha hizo jambo ambalo ni kinyume na makubaliano na kwamba inachangia ukatili kwa watoto kwani hawapewi chakula kizuri. Ulimbakisya Mbuto Mchungaji wa Kanisa la Moraviani Ushirika, amesema hakuwahi kukaa meza moja pamoja na mkewe kutengeneza bajeti badala yake alimtegemea mkewe kuendesha familia. Amesema hakuwahi kumpa mkewe hela ya mtaji kwa ajili ya biashara na kwamba laiti angepata elimu ya upangaji bajeti mapema angepiga zaidi hatua za maendeleo. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Godfrey Kingamkono, amesema katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2020 hadi Juni 2021 Halmashauri imetoa mikopo kwa vikundi 70 yenye thamani ya shilingi 420. Amesema vikundi vilivyonufaika ni vya wanawake 28 vimepata shilingi 168 wakiwemo wafanyabiashara na wanaonza kujishughulisha kupitia fedha hizo. Vilevile vikundi vya vijana 26 kupatiwa shilingi 168 na vikundi vya wenye ulemavu 16 vikipatiwa shilingi 84. Hata hivyo Mkoa wa Mbeya kupitia Kamati yake ya Ushauri katika Mwaka wa fedha 2020/2021 kwa Wilaya ya Kyela imepanga kutumia shilingi 252 kwa kuvinufaisha vikundi 26, wanawake vikundi 10, vijana vikundi 10 na watu wenye ulemavu vikundi sita. Katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya, jumla ya vikundi 150 vya wanawake wametengewa fedha kiasi cha shilingi milioni 422 na fedha zote tayari zimetolewa kwa vikundi hivyo. Katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe jumla ya vikundi vya wanawake 17 vimenufaika na mkopo wenye thamani ya shilingi milioni 334. Kwa Mujibu wa Ofisa ya Maendeleo ya jamii, Mkoa wa Mbeya, Stella Kategile amesema hadi kufikia Disemba 2020 jumla ya vikundi 94 vya wanawake vimepatiwa mikopo ya asilimia kumi ya mapato ya ndani kiasi cha shilingi milioni 571.  

Add a Comment

Your email address will not be published.

All Categories

Get Free Consultations

SPECIAL ADVISORS
Quis autem vel eum iure repreh ende