Marekebisho sheria ya ndoa, maoni yaendelea kukusanywa

Na Mwandishi Wetu, Dodoma Timu ya wataalam iliyoundwa na Wizara ya Katiba na Sheria kwa ajili ya kukusanya maoni kuhusu marekebisho ya Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, ipo katika mikoa minne nchini ikiwemo Dar es Salaam kukusanya maoni. Mikoa mingine ambayo timu hiyo inakusanya maoni ni Tanga, Mtwara na Lindi ambapo imekuwa ikukutana na makundi mbalimbali. Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Damas Ndumbaro amesema timu hiyo inaendelea kupokea maoni ya wananchi kuhusiana na mapendekezo ya marekebisho ya sheria kupitia dodoso lililoandaliwa ili kuwa na uelewa wa pamoja. “Kwa sasa wizara inaendelea na ukusanyaji wa maoni ambapo imeendelea kukutana na wadau na makundi mbalimbali yakiwemo; kamati ya bunge ya kudumu ya katiba na sheria, wabunge, viongozi wa dini, viongozi wa kimila, waendesha piki piki maarufu kama boda boda,”amesema. Amewataka Watanzania kuwa watulivu na zoezi linaoendelea kutekelezwa na wizara la kukusanya na kuchambua maoni na amesema likikamilika wizara itawasilisha bungeni mapendekezo ya sheria hiyo kwa ajili ya kujadiliwa na hatimaye kupitishwa,”amesema. Kufanyiwa marekebisho kwa sheria hiyo kunatokana na uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wa kutaka Sheria ya Ndoa kupitiwa upya ili kuondoa ubaguzi na kukosekana kwa usawa kati ya umri wa chini wa ndoa kwa wavulana na wasichana. Uamuzi huo unatokana na kesi iliyofunguliwa na mwanaharakati Rebecca Gyumi dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu umri wa kuolewa na kuoa.

Add a Comment

Your email address will not be published.

All Categories

Get Free Consultations

SPECIAL ADVISORS
Quis autem vel eum iure repreh ende