Undeni vikundi iwe rahisi kupata mikopo, wanawake waaswa
Na Mwandishi Wetu, Njombe
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Njombe, Beatrice Malekela amewashauri wanawake kujiunga kwenye vikundi ili wanufaike na fursa mbalimbali za kiuchumi, ikiwemo mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri .
“Nawaambia wanawake wawe na uthubutu, uthubutu wa kuanza,bila kusikiliza maneno ya watu… mwanamke hutakiwi kubabaika unapofanya kazi…piga pamba,endelea na kazi na watu wataona, imani huzaa imani” amesema wakati akiongea na waandishi wa habari.
Vilevile amewaasa kutumia taaluma zao kuisadia jamii ikiwemo katika kutatua migogoro, kusimamia maadili pamoja na kuibua miradi mbalimbali itakayowasaidia kujitegemea kiuchumi ili kuwa na familia imara pamoja na jamii yenye mafanikio.
Katika hatua nyingine, Beatrice amewaomba wanawake wilayani Njombe kuacha kutumika na viongozi mbalimbali ili kuleta maendeleo katika jamii.
Amesema, maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo wanawake wamekuwa wakishawishika kufanya mambo yasiyofaa kwa kuahidiwa kupewa fedha ,msaada au nafasi za uongozi, jambo linalozorotesha maendeleo katika maeneo yao .
Aidha amesema hali hiyo inajitokeza hata katika chaguzi mbalimbali ambapo baadhi ya wanawake wanarubuniwa kuchagua viongozi wasio na maono ambao wanataka nafasi hizo kwa manufaa yao wenyewe na si kwa ajili ya kutatua changamoto zinazoikabili jamii inayowazunguka.
Amesema kabla hawajafanya maamuzi ya jambo lolote wanatakiwa kupima faida na hasara yake ili wasije kuharibikiwa na baadaye kupata majuto
Mwenyekiti Beatrice amewaonya pia kuhusu tabia za kutaka mafanikio ya haraka na akawasisitiza kuwa na bidi ya kazi na kuongeza ubunifu katika shughuli wanazozifanya.
Beatrice ni Mwenyekti wa UWT katika wilaya ya Njombe yenye kata 37 na matawi ya CCM 207. Yuko katika muhula wa pili wa uongozi utakaoishia mwaka 2027.
Recent Posts
admin0 Comments
Heavy rains raises concerns
Joyce Bazira0 Comments
Siku ya Wazee Dunia; Tanzania ina mengi ya kujivunia?
Joyce Bazira0 Comments