Malindi Estate waandaa matembezi kuhimiza watu kushiriki Sensa
Na Sabina Ntobi
Uongozi wa Serikali ya mtaa Malindi Estate, Kinondon Jijini Dar es Salaam, umeandaa matembezi ya hiari kwa ajili ya kuhimiza wananchi wa maeneo hayo kushiriki kikamilifu kwenye zoeli la Sensa ya Watu na Makazi.
Mwenyekiti wa mtaa huo,Clement Mshana amesema matembezi hayo
yatafanyika Agosti 20 mwaka huu, kuanzia saa kumi na moja alfajiri na
yataanzia eneo zinapojengwa ofisi za Serikali ya mtaa, barabara ya
Flamingo na Obama,Mbweni na kuishia Uwanja wa Ubungo,Mbweni.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mtaa ,mgeni rasmi wa shughuli hiyo
atarajia kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Akifafanua zaidi, Mshana amesema dhumuni la hayo matembezi ni kutoa elimu kwa wananchi juu ya masuala mbalimbali yanayohusiana na sensa.
Aidha,amesema baada ya matembezi hayo, wananchi watapewa ufafanuzi kuhusu viambatanisho vinavyohitajika wakati wa sensa na maswali muhimu yatakayoulizwa wakati wa zoezi hilo ili kuwaandaa wananchi na ili kuzuia kupoteza muda.
Zoezi la sensa ya watu na makazi litafanyika Agosti 23, 2022 nchini kote kwa lengo kufahamu idadi kamili ya watu na kuweka bajeti inayotosha kwa ajili ya wananchi wote na maendeleo yao.
Recent Posts
admin0 Comments
Heavy rains raises concerns
Joyce Bazira0 Comments
Siku ya Wazee Dunia; Tanzania ina mengi ya kujivunia?
Joyce Bazira0 Comments