Wasichana wanaosoma sayansi vyuo vikuu kufadhiliwa
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Wasichana 244 kati ya 640 waliopata alama za ufaulu wa juu katika mitihani yao ya kidato cha sita na kudahiliwa kusoma masomo ya sayansi vyuo vikuu, watanufaika na ufadhili wa Samia Scholarship katika mwaka 2022/2023.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda anasema wanafunzi hao watalipiwa ada ya mafunzo, posho ya chakula na malazi.
Mambo mengine watakayolipiwa ni mahitaji muhimu ya vitivo, mafunzo kwa vitendo, utafiti, vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum na bima ya afya.
“Samia Scholarship itagharamia kwa asilimia 100 masomo ya Chuo Kikuu kwa wanafunzi ambao wamepata udahili katika fani za teknolojia, uhandisi, hisabati na tiba,”amesema.
Profesa Mkenda amesema lengo la ufadhili huo ni kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 ya kuendeleza sayansi na teknolojia.
Profesa Mkenda amesema katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imetenga Sh3 bilioni kwa ajili ya ufadhili huo ambao utaendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka.
Recent Posts
admin0 Comments
Heavy rains raises concerns
Joyce Bazira0 Comments
Siku ya Wazee Dunia; Tanzania ina mengi ya kujivunia?
Joyce Bazira0 Comments