0
Your Cart
No products in the cart.

Wasichana wanaosoma sayansi vyuo vikuu kufadhiliwa

Na Mwandishi Wetu, Dodoma Wasichana 244 kati ya 640 waliopata alama za ufaulu wa juu katika mitihani yao ya kidato cha sita na kudahiliwa kusoma masomo ya sayansi vyuo vikuu, watanufaika na ufadhili wa Samia Scholarship katika mwaka 2022/2023. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda anasema wanafunzi hao watalipiwa ada ya mafunzo, posho ya chakula na malazi. Mambo mengine watakayolipiwa ni mahitaji muhimu ya vitivo, mafunzo kwa vitendo, utafiti, vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum na bima ya afya. “Samia Scholarship itagharamia kwa asilimia 100 masomo ya Chuo Kikuu kwa wanafunzi ambao wamepata udahili katika fani za teknolojia, uhandisi, hisabati na tiba,”amesema. Profesa Mkenda amesema lengo la ufadhili huo ni kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 ya kuendeleza sayansi na teknolojia. Profesa Mkenda amesema katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imetenga Sh3 bilioni kwa ajili ya ufadhili huo ambao utaendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka.

Add a Comment

Your email address will not be published.

All Categories

Get Free Consultations

SPECIAL ADVISORS
Quis autem vel eum iure repreh ende